MAGITA KUISHIKA MKONO TASNIA YA FILAMU NCHINI , YAMWAGA MADOLA KUISAIDIA SINGLE ZERO
Na: Imani Kelvin Mbaga, Dar es salaam.
Tasnia ya filamu nchini imeingia katika ukrasa mpya baada ya kupata uungwaji mkono toka kwa wadau walio na nia ya kuipeleka tasnia hiyo mbali na kuifanya kuwa sekta muhuimu kwa taifa huku ikitarajiwa kuajiri maefu ya vijana na kupunguza tatizo la ajira katika jamii.
Hayo yamebainika jana wakati wa hafla ya kuzindua filamu mpya ya Kitanzania iliyopata tuzo huko huko nchini Marekani na inayotarajiwa kuwa moja ya filamu zitakazotikisa anga la filamu hapa nchini, na kulenda mapinduzi makubwa katika sekta hiyo.
Filamu hiyo iitwayo SINGLE ZERO iliyochezwa na msanii maarufu wa filamu nchini , Tino Muya, ilizinduliwa jana chini ya udhamini mnono wa kampuni ya MAGITA Investment, ambayo licha ya kudhamini shughuli za uzinduzi huo, pia mkurugenzi wake bw, Magita alinunua DVD mja kwa dola 5000 za Kimarekani.
Akiongea muda mfupi kabla ya uzinduzi huo mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema wanafikiria kuboresha namna ya kuinua na kuipeleka mbele tasnia ya filamu nchini, kwakuwa imeonyesha kuwa ni sekta ambayo endapo itashikwa mkono basi inaweza kuinua pato la taifa na mwananchi mmoja mmoja.
"Nimefurahi kuona vijana wa Kitanzania wakifanya kazi kwa bidii na kupata mafanikio bila kusaidiwa, sisi tumekuja kufanya mabadiliko katika sekta hii, na ndo kwanza tunaanza kuisadia tasnia hii lakini watu watarajie mambo makubwa zaidi yanakuja" Alisema Mkurugenzi huyo
Kampuni ya MAGITA inayojihusisha na masuala ya bima za aina zote, pamoja na shule ya udereva wa magari, imejikita katika kusaidia tasnia hiyo ya filamu nchini, kwa kudhamini tukio la kipekee la uzinduzi wa filamu kama inavyofanyika katika nchi zilizoendelea.
Aidha kampuni hiyo imefanikiwa kuwaunganisha wasanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya, ambao ni Tino Muya na Ben Paul ambao kwa sasa watakuwa chini ya usimamizi wa kampuni hiyo ya MAGITA investment na tayari wasanii hao wameahidi kushirikiana katika kazi zao.
Naye Tino Muya ambaye ni mchezaji mkuu katika filamu hiyo, aliushukuru uongozi wa kampuni ya MAGITA, kwa kumuunga mkono katika harakati za kuinua tasnia hiyo na kuifikisha mbali hususani katika anga za kimataifa na kuleta heshima hapa nchini kwa jumla
| Tino Muya akionyesha tuzo aliyopata kupitia filamu yake ya SINGLE ZERO, tuzo zilizopatikana nchini Marekani |
| Tino Muya akiwa n wasanii wake akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani y dola za Kimarekani 5000 |
| Baadhi ya wasanii wa filamu pamoja na Tino Muya wakiwa wameshikilia mfano wa cheki yenye thamani ya dola 5000 iliyotolewa na kampuni ya bima ya MAGITA |
| Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Bernad Paul, maarufu kama Ben Pol akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo |
| Tino Muya akiwa pamoja na msanii mwenzake wa filamu Michael Duma wakati wa uzinduzi wa filamu ya SINGLE ZERO |
Post a Comment