Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

TANZANIA YAIPANIA OLIMPIKI 2020 TOKYO JAPAN

mkurugenzi wa michezo nchini, Omar Yusuph akitoa hotuba fupi wakati wa uzinduzi wa mpango wa kushiriki Olimpiki 2020 itakayofanyika Tokyo Japan


 Na Imani Kelvin Mbaga, Dar es salaam.




Shirikisho la soka nchini Tanzania limezindua mpango mkakati utakaoiwezesha Tanzania kupeleka timu ya mpira wa miguu kushiriki michuano ya Olimpiki 2020 inayotarajiwa kufanyika katika jiji la Tokyo nchini Japani.

Mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi wa michezo nchini,  Omar Yusuph, kwa niaba ya serikali alisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na shirikisho la soka nchini katika kuhakikisha kuwa kuna maendeleo yanayofikiwa katika soka.

“Serikali inawapongeza sana, na inaahidi kuwaunga mkono katika kazi zenu, huku tukitanbua kuwa katika mchezo wowote bila ya kuanza na vijana hatuwezi kupata maendeleo” Alisema mkurugenzi huyo

Akizungumza awali wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es salaam leo, Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi, alisema mpango huu unajumuisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 15, 17 na 19 ambao wanafuzu kucheza michuano hiyo.


Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF)

“Tunashukuru kwamba tumefikia siku hii muhimu ambapo kama Watanzania wapenda soka tunajumuika kushudia kuanza safari ya pamoja kuelekjea kutimiza ndoto zetu” Alisema Malinzi

“Tumefanya juhudi kubwa na tunaomba kungwa mkono na wadau wote kwani ni gharama kubwa kuendesha mpira hasa soka la vijana, hata hivyo tumejizatiti ili kuhakikisha kuwa ndoto zetu zinafanikiwa” Aliongeza.

Naye mshauri wa soka la vijana nchini , Kim Polsen alisema kuwa mpira ni safari, na safari siyo hatima bali ni mwendo unao taka moyo wa kupambana, na aliipongeza TFF kwa kuanza safari hiyo kuelelekea Tokyo mwaka 2020


Mshauri wa soka la vijana nchini Kim Poulsen


“Nimefurahi kuhudhuria uzinduzi huu muhimu sana kwa hatima ya soka la Tanzania, nimefurahi pia kuwaona vijana wadogo ambo tumekuwa tukiwajenga kwa muda sasa ambao ninaamini watakuja kuwa wakombozi wa soka letu” Alisema Polsen




Wageni mbalimbali maarufu walikuwepo kwenye uzinduzi huo wakiwemo, Makamu wa Rais wa kamati ya Olimpiki Tanzania, Henry Tandau, mwenyekiti wa soka la vijana ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Dodoma, Mlamu Ng’ambi, kocha wa timu ya taifa Salum Mayanga na wengine wengi.






Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Selestine Mwesiga



Makamu wa Rais wa kamati ya Olimpiki Tanzania, Henry Tandau akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ushiriki wa timu ya mpira wa miguu katika michuano ya Olimpiki 2020 Tokyo Japan


Mkurugenzi wa michezo nchini, Omar Yusuph akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa kampeni ya kushiriki michuano ya Olimpiki 2020 Tokyo Japan

Viongozi, wachezaji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kushiriki michuano ya Olimpiki 2020 wakiwa kwenye picha ya pamoja katika uwanja wa karume jijini Dar es salaam

vijana wa serengeti boys wakifanya mazoezi uwanja wa karume jijini Dr es salaam

No comments

Powered by Blogger.