SERIKALI YAMPONGEZA DIAMOND NA KUMKABIDHI BENDERA
| Waziri Nape Nnauye (picha na Imani Kelvin Mbaga) |
Na: Imani Kelvin Mbaga, Dar es salaam.
Waziri wa habari, vijana, utamaduni, sanaa na michezo, mhe, Nape Nnauye, amesema serikali itajitahidi kufanya kila linalowezekana ilimkuifanya sekta ya sanaa nchini inakuwa tegemeo kwa vijana wa kitanzania ikiwa ni pamoja na kuzalisha ajira kwa vijana wengi kadri iwezekanavyo.
waziri nape aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya kumpongeza mwanamuziki Diamond platnums aliyeteuliwa kwenda kutumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa michuano ya kombe la mataifa barani Afrika, AFCON, itakayofanyika nchini Gabon kuanzia tarehe 14 ya mwezi huu.
| Alpha Mria, meneja masoko wa kampuni ya Multchoice Tanzania (picha na Imani Kelvin Mbaga) |
"Tunatambua mchango wa wasanii wetu katika kuitangaza nchi yetu na tunawaunga mkono kila inapobidi, lakini pia tutafanya kila liwezekanalo ili kuwatengenezea mazingira bora kwakuwa tunajua pia kwamba sanaa imekua ajira kwa vijana wetu" Alisema waziri Nape
"Nampongeza Naseeb na kundi lake la WCB ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kukuza muziki wetu na kuitangaza nchi kwa jumla, na leo niliona vyema nifike mwenyewe kuja kushuhudia na kumkabidhi bendera na pongezi kwa kutuwakilisha vema" Aliongea Waziri Nape
Akimkaribisha mhe, Waziri, kaimu mkurugenzi wa kampuni ya Multchoice Tanzania, Salum Salum, ambao ndiyo waliokuwa waandaji wa hafla hiyo, alisema kuwa kampuni yake kupitia king'amuzi chao cha DStv wanatarajia kuonyesha michezo yote ya AFCON na wateja wao wataiangalia michezo hiyo kwa bei ya kawaida ya malipo ya kifurushi chao cha DStv bomba.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na balozi wa kifurushi cha DStv bomba, msanii wa maigizo nchini Tanzania anaejulikana kwa jina maarufu la JOTI
| Salum Salum, kaimu mkurugenzi wa kampuni ya Multchoice Tanzania (picha na Imani Kelvin Mbaga) |
Post a Comment