TANZANIA MDOMONI MWA UGANDA KUFUZU AFCON 2019
![]() |
| Taifa Stars |
Na: Imani Kelvin Mbaga
Hatimaye shirikisho la soka barani Afrika "CAF" limeweka hadharani makundi kwa ajili ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2019 zitakazo chezwa Cameroon, na kuiangushia Tanzania mikononi mwa wababe wa ukanda wa Afrika Mashariki na kati, timu ya taifa ya Uganda "the Uganda Cranes"
Katika orodha iliyotolewa jana na shirikisho hilo, kutakuwa na jumla ya makundi kumi na mawili, huku kila kundi likipeleka timu moja itakayoibuka kinara wa kundi lake, mwenyeji pamoja na timu tatu zitakazo maliza katika nafasi ya pili kwa uwiano bora zitakamilisha idadi ya ya timu 16 zitakazocheza fainali hizo
Kwa mujibu wa orodha hiyo Tanzania ipo katika kundi L pamoja na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho ambzo zinakamilisha idadi ya timu nne zinazopaswa kuwepo katika kila kundi.
Kundi hili lina timu ambazo zinaizidi Tanzania katika msimamo wa ubora wa soka unaotolewa la shirikisho la soka ulimwenguni FIFA, ambapo kwa mujibu wa msimamo wa mwezi Januari mwaka huu, Uganda inashika nafasi ya 18 kwa ubora wa soka barani Afrika.
Timu nyingine ni Cape Verde inayoshika nafasi ya 19, Lesotho inashika nafasi ya 43 wakati Tanzania ikishika nafasi ya 48 kwa ubora wa soka hapa barani Afrika.
Tanzania imesha wahi kuwa kwenye kundi moja na Cape Verde kabla visiwa hivyo havijafanya mapinduzi makubwa ya soka, takribani miaka kumi iliyopita na Tanzania kupata pointi nne kwa kutoka nao sare uwanja wa Taifa kabla ya kuwabamiza 4-0 wakiwa kwao.
hata hivyo baada ya hapo visiwa hivyo vimefanya mapinduzi makubwa na kwa kipindi hicho waliweza kupata nafasi ya kuiwakilisha Afrika kwemnye kombe la Dunia lililochezwa Brazil licha ya kunyang'anywa nafasi hiyo kwa kuchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Timu hiyo pia imeweza kupata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mara mbili, wakati ambapo Tanzania ilibaki palepale na kuendelea kuporomoka kisokam kila siku.
Uganda imekuwa ikiisumbua sana Tanzania katika miaka ya hivi karibuni, ikikumbukwa kuwa wamewahi kuiondoa Taifa Stars katika michuano ya CHAN mara mbili, na katika fainali za mwaka huu
Bila shaka hili si kundi rahisi kwa taifa Stars, kinachosubiriwa ni kuona mikakati ya shirikisho la soka la Tanzania "TFF" kuelekea kufuzu kwa fainali hizo.
Makundi mengine kama yalivyotolewa na CAF hapo jana ni kama inavyoonekana hapo chini
(imeandaliwa na Imani Kelvin Mbaga wa Tanganyika blog)


Post a Comment