NBC YAWAPONGEZA WAFANYAKAZI WAKE BORA
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la
Corporate, Mariam Kombo (kushoto), akionyesha cheti alichotunukiwa mara
baada ya kutangazwa meneja bora wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake
mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Kulia ni
Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi. Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja wa Kanda wa Benki ya NBC
James Ndimbo (kushoto), akionyesha cheti mara baada ya kutangazwa meneja
bora wa kanda wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika
sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Katikati ni Mkurugenzi wa
Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi na kulia ni mkuu wa
idara ya Biashara NBC Elvis Ndunguru. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar
es Salaam hivi karibuni.
Meneja wa amana za wateja NBC,
Dorothea Mabonye (kushoto), akikabidhi kombe la ushindi kwa Meneja wa
Tawi la NBC Sea Cliff baada ya tawi hilo kuibuka kidedea katika kutoa
huduma za kibenki kwa wateja wa akaunti ya malengo kwa mwaka 2016 .
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa idara ya mikopo binafsi
wa NBC, Andrew Lyimo, akimkabidhi kikombe cha ushindi meneja wa tawi la
Samora, Faustina Maeda (katikati) aliyeibuka kidedea katika utoaji wa
mikopo kwa watu binafsi katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi
bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mtenya Cheya, meneja mikopo kwa watu
binafsi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBC,
Mongateko Makongoro (mwenye suti nyeusi) akipiga picha ya pamoja na
washindi wa tuzo ya utoaji wa mikopo binafsi walioingia kwenye Kundi la
Watu Mashuhuri wa NBC lijulikanalo kama ‘ ‘Kundi la Shilingi Billioni
Moja’. Tuzo hizo zilitolewa kwenye sherehe maalum ya kuwatunuku
watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Huduma Reja Reja za
Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), akipiga picha ya
pamoja na baadhi ya wafanyakazi bora waliofanya vizuri katika mwaka 2016
walio chini ya kurugenzi yake, katika sherehe maalum ya kuwatunuku
watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.
Post a Comment