Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

AGENDA: TUNAHITAJI KIWANGO CHA MADINI YA RISASI KATIKA RANGI HAPA TANZANIA

Na Frank C Gibebe

Asasi  ya AGENDA Inayojihusisha na mazingira na maendeleo  pamoja na  Asasi ya kutetea walaji Tanzania {TCAS} Kwa pamoja wamelitaka shirika la viwango Tanzania {TBS} Kuweka viwango vya madini ya risasi katika Rangi ambapo viwango hivyo ni muhimu kuondoa rangi zenye ya risasi zinazotengenezwa, kuingizwa ,kuuzwa na kutumika nchini.


Prof.Jamida Katima,  Mwenyekiti AGENDA.

Wito huo umetolewa  mapema leo hapa jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  wiki ya kimataifa kujikinga na madhara ya madini Risasi ambayo yanafanyika duniani kote kuanzia tarehe 23-29 oktoba  2016 na kuratibiwa na programu ya mazingira ya umoja wa mataifa [UNEP} Na shirika la Afya Duniani [WHO}

Akizungumza na waandishi  wa habari katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa bodi ya AGENDA Prof.Jamidu Katima, wa chuo kikuu cha Dar es salaam, amesema madhara ya kiafya yanayosababishwa na madini ya risasi katika ubongo wa mtoto mdogo ni ya kudumu na hayawezi kurekebishwa wala kutibika.
“Tunakwamisha maendeleo ya kiakili ya watoto wetu na ya taifa kwa ujumla ijapokuwa mibadala salama ya madini ya risasi ambayo ni nafuu inapatikana na kutumika nchini kwetu Tanzania, ni lazima tupunguze chanzo hiki cha madhara ya madini ya madini risasi kwa watoto wadogo” Alisema Prof Katima.
Wadau wakifatilia mjadala

Bi Dorah Swai , afisa mipango wa AGENDA akichangia Mada


Kwa upande mwingine Prof.Kitima, Amesema Watoto wadogo hasa walio chini ya miaka sita hula au kuvuta vumbi lenye rangi yenye madini hayo na kwa tabia ya watoto kuingiza mikono kinywani au wanapolamba au kutafuna midoli ,samani za nyumbani au vitu vingine vilivyopakwa rangi yenye madini ya risasi ambapo ndio mwanzo wa kuathirika

Ameeleza kuwa serikali inapaswa kuweka na kusimamia utekelezaji wa viwango vya udhibiti wa madini ya risasi katika rangi lakini viwango vya uzalishaji rangi havihitaji kusubiri viwango,bali vinatakiwa kuanza kupunguza  viwango vya madini ya risasi kuanzia sasa
.
Aidha katika taarifa iliyoandaliwa kwa mwaka huu kwa ajili  ya wiki ya kimataifa ya kujikinga na Madhara ya madini ya risasi , Mkurugenzi wa idara ya afya ya jamii na Mazingira ya shirika la Afya Duniani {WHO} Dk.Maria Neira  “kuingiwa na madini ya risasi mwilini kunasababisha madhara makubwa kwa Afya ya binadamu hususani kwa watoto wadogo, Hakuna sababu ya kuongeza madini ya risasi katika rangi , kemikali  mbadala zilizo salama zinaweza kutumika. Njia bora za kuhakikisha rangi zisizokuwa na madini ya risasi zinapatikana ni kwa nchi kuweka sheria , kanuni au viwango vya lazima vinavyodhibitiwa uzalishaji , usambazaji, uuzaji au utumiaji wa rangi zenye madini ya risasi”
Silvan Mnganga, Afisa Mipango Mkuu AGENDA

Hata hivyo Pamoja na tafiti zilizofanyika Tanzania kuonesha kuwa rangi nyingi za mafuta zinazozalishwa ,kuingizwa na kutumika nchini zina viwango vikubwa vya madini risasi nyingine kufikia kiwango cha sehemu 99,000 ya milioni {99,000ppm} bado nchi haina sheria rasmi au viwango vya lazima vya kudhibiti madini ya risasi karika rangi

Dorah Swai ambaye ni Afisa Mipango wa AGENDA Anasema zipo hatua zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kuwa na viwango, Hivyo ameiomba serikali kupitia shirika la viwango yaani TBS Kuharakisha kupitishwa na kutumika kwa viwango hivyo.
Wafanyakazi wa Agenda kazini

PICHA YA PAMOJA NA WADAU


Waandishi wa habari wakifatilia kwa makini

No comments

Powered by Blogger.