HUENDA MAFANIKIO HUPATIKANA KWA KILE ANACHOKIAMINI MTU NA KUKIPIGANIA KWA NGUVU ZOTE
MSANII SIR KING |
Kila mtu ana njia yake hapa duniani ndio neno ninaloweza kusema
kwa wadau wangu na wasomaji wa tanganyikaradio.blogspot.com,
kwa kuwa kila mmoja wetu hupata mafanikio kwa kile anachokiamini na kukipigania
kwa nguvu zote ili mradi atimize kile kinachompa nguvu kuhusu jambo hilo.
Leo katika pita pita za huku na kule ndipo nimekutana na kijana anaefahamika
kwa jina la Sir King mkazi wa mabibo
jijini dar es salaam, mwenye kila sababu ya kutimiza ndoto zake kutokana na
kuelekeza nguvu kubwa kwa mambo anayo yaamini.
Sir King akiongea na mwandishi wa makala
haya anasema alianza kujigundua kuwa na kipaji cha kuigiza tangia akiwa shule
ya msingi mkoani manyara na alikuwa akitamani sana kuja kuwa muigizaji mkubwa
hapa nchini.
Pindi alipo maliza elimu ya sekondari alijiingiza katika sanaa ya
uigizaji rasmi mwaka 2009 hapa jijini dar es salaam, kwa kuanza kuigiza mitaani
na marafiki zake na baadae kupata kundi la K
Film Production lenye maskani yake Tabata Sheli.
Mwaka huo huo baada ya kujiunga na kundi hilo alifanikiwa kucheza
movie tatu ikiwemo Beijing, Funzo la ndoa, The camp site na ya nne amecheza mwaka
huu mwanzoni inaitwa Chura, ambayo baada ya msanii wa bongo movie na msanii wa
bongo fleva Snura Mushi kuachia
wimbo wake wa chura.
Baada ya kucheza movie nne, Sir
King ameona akiwa na malengo ya
kufika mbali katika tasnia ya filamu hapa nchini ni bora na yeye akafata njia
wanazopita wasanii wenzake wa filamu hapa nchini za kuingia katika upande wa
muziki.
Katika upande wa muziki amejiingiza rasmi mwaka jana 2015, na
kubwa lililomsukuma kuingia katika upande wa pili wa muziki ni kipaji cha
kuimba kwani amekuwa mwalimu wa kwaya kanisani kwa kipindi kilefu na wengi
waliofundihswa nae kwaya kanisani wamekuwa wakikubali uwezo wa mwalimu wao.
Na tangu ajiingize rasmi katika muziki tayali ameshatengeneza
nyimbo tatu ambayo ya kwanza ameitengeneza mwaka jana katika studio za mazuu
chini ya mtayarishaji mazuu inayotambulika kwa jina la wewe ni uhai moyoni
mwangu ambayo amemshirikisha msanii mwenzake PNC, na ulipata muda mwingi hewani katika vituo mbalimbali vya
radio, magazeti na mitandao ya kijamii.
Kufanya vizuri kwa wimbo huo kukampa moyo wa kutengeneza wimbo
mwingine wa pili uliotambulika kwa jina la nitalia ambayo ameitayarisha katika
studio mbili tofauti ya kwanza iliyotengeneza beat ni mazuu na kukamilishwa na
studio ya G records chini ya
mtayarishaji KGT.
Wimbo huu wa pili pia ilitanua wigo wa kusikika katika vyombo
mbalimbali vya habari na kufanikiwa kufanya matamasha mbalimbali jijini dar es salaam
na mikoa mbalimbali, zilizomuingizia fedha kiasi za kuendesha maisha yake.
Kwa sasa yuko mbioni kuachia wimbo mwingine wa tatu unakwenda kwa
jina la wote marafiki, umetayarishwa katika studio za Sadactive chini ya
mtayarishaji Double B ambayo itaachiwa muda si mrefu kabla ya kuisha kwa mwaka
huu.
Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini, kuweza
kumshika mkono katika kuhakikisha anatimiza ndoto zake kwa kuwa na wasimamizi
wazuri wataofanya kazi pamoja na kufikia malengo yake, pamoja na wasanii
wakubwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wanaochipukia ili kuujenga mziki wetu
kitaifa na kimataifa, kwani muziki wetu umekuwa na wasanii wachache hivi sasa
wanaoiwakilisha nchi kimataifa tofauti na nchi kama Nigeria na Afrika ya
kusini.
Anasema kutokana na wasanii wakubwa kutoawangalia wakubwa utakuta
hata katika tuzo wanazochaguliwa unakuta wamezungukwa na wasanii wengi wa
Nigeria au Afrika ya kusni, nah ii ni kutokana na wao kuwa wachache tofauti na
wenzetu kugeana ushirikiano kikubwa wanachoangalia ni muziki wao kusonga mbele
kimtaifa.
Jumanne juma
0658-291940
Post a Comment