HATIMAYE LIGI YA WANAWAKE KUANZA RASMI
Na: Imani Kelvin Mbaga
Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limetangaza kuanza
rasmi kwa mashindano ya ligi kuu ya wanawake nchini Tanzania ambayo yanatarjiwa
kuanza rasmi tar mosi Novemba kwa
uzinduzi utakaofanyika mjijini Dodoma siku hiyo.
Akizungumza na
waandishi wa habari makao makuu ya
shirikisho hilo Karume jijini Dar es salaam leo, Alfred Lucas ambaye ndiye
msemaji wa shirikisho, alisema ligi hiyo imepangwa kuanza kama ilivyokusudiwa na kuwa
usajili wa wachezaji utabaki kama ulivyo kwakuwa hakukuwa na uthibitisho juu ya
madai ya vilabu vilivyokata rufaa juu ya usajili.
“kama tulivyosema
hapo mwanzo kuwa ligi kuu ya mpira wa miguu kwa upande wa akina dada itaanza
tar moja Novemba na uzinduzi wake utafanyika
mjini Dodoma, kwa tamngazo hili pia wale waliokataa rufaa wajue kuwa rufaa zao
zimetupwa kwakuwa hazikuwa na vielelezo muhimu hivyo usajili utabaki kama
ulivyo” Alisema Lucas.
Kwa mujibu wa ratiba
siku ya ufunguzi inaonyesha kuwa kuwa kutakuwa na mechi kati ya Bawbab ya
Dodoma watakaoingia dimbani kucheza na Panama fc kutoka Iringa .
Naye Baruan Muhuza
mkurugenzi wa michezo wa kampuni ya utangazaji ya Azam ambao ndiyo wenye hgaki
ya kuonyesha michuano hiyo, alisema kuwa wao wamejipanga kuonyesha michezo
mitatu kila siku ya mechi hizo na
kwamba wana uhakika wataonyesha bila kuwa
na wasiwasi na kwa ufanisi mkubwa kama ilivyo kwe ligi kuu ya Vodacom.
“Tumejipanga
kuonyesha mechi tatu kati ya nne zitakazokuwa zinachezwa kwa ubora ule ule na
tunafurahi kuwa hii itakuwa ni ligi ya kwanza ya wanawake katika ukanda huu wa
Afrika Mashariki kwakuwa hakuna nchi yenye ligi ya
wanawake kama itakavyokuiwa kwetu, nasi tutaonyesha michezo hiyo kama
tufanyavyo kwa wanaume” Aliserma Muhuza
Akizitaja sababu za kupeleka ufunguzi wa ligi hiyo mjini
Dodoma , Muhuza alisema, wameamua kupeleka huko kama sehemu ya kuunga mkono
hatua ya serikali kuhamia Dodoma lakini
pia michuano hiyo itachezwa wakati vikao
vya bunge vikiwa vinaendelea na hivyo
viongozi wengi wa serikali pamoja na wabunge walioko Dodoma watapata fursa ya kushuhudia sherehe
hizo za kihistoria za ufunguzi wa michuano hiyo.
Hii itakuwa ni ligi kuu ya kwanza ya wanawake kuchezwa
katika ukanda wa CECAFA, huku shikisho la soka hapa nchini likikusudia kuiotumia
michuano hiyo kama sehemu ya kuimarisha vikosi vya timu za taifa za wanawake
hapa nchini.
waandishi wa habari za michezo na wapiga picha makao makuiu ya TFF jijini Dar es salaam leo |
Post a Comment