MARATHONI YA UBINGWA WA VPL NDO INAANZA RASMI
Na: Imani Kelvin Mbaga
Ligi kuu ya Voadacom Tanzania bara tayari inaonekana kugeuka
na kuwaacha mafahali wawili wa soka hapa nchini kuanza mbio za marathoni
kuelekea kwenye ubingwa wa ligi hiyo. Kwa matokeo ya hivi karibuni kwa timu
zote inaonyesha kuwa Simba na Yanga tayri wamesha jitenga na wenzao na
kufukuzana wenyewe kuelekea ubingwa wa ligi hiyo na wengine wakioekana kana
kwamba wameshakata pumzi.
Simba wanaongoza wakiwa na
jumla ya pointi 29 huku wakiwa pointi
tano juu ya watani wao wa jadi Yanga wenye pointi 24 katika nafasi ya pili.
Yanga ambao ni kama hawakuanza mbio hizi kwa nguvu sasa wanaonekana kuwa katika
“fom” ya ajabu baada ya kutikisa nyavu mara kumi katika mechi mbili pekee tena
mechi zilizotabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kwao.
Pamoja na yote
tuwezayo kusema hatuwezi kuacha kuzungumzia watikisa nyavu wanaoziweka timu hizo
kileleni mpaka sasa kwa magoli yao. Wachezaji wanane tu wa vilabu hivi viwili
wametikisa nyavu mara 39 kwa pamoja wakati ambapo wale wa Yanga wametikisa
nyavu mara 20 na wenzao wa Simba wametikisa nyavu mara 19.
Shiza Kichuya ni mchezaji aliyetajwa kwa kusifiwa mara
nyingi zaidi na inawezekana kungekuwa na kura za mtandaoni bila shaka angeibuka
kuwa mchezaji maaarufu na anyependwa hadi sasa anaongoza orodha ya wafungaji
kwa kupachika wavuni magoli 7.
Wakati Kichuya akiongoza kw umaarufu huo mchezaji mwenzakw
Obrey Chirwa Mzambia anyechezea mabingwa
watetezi, Yanga Sc aliongoza kwa kukejeliwa
na kuitwa majina ya ajabu kwa kutofanya vizuri mwanzo wa msimu llakini hali
hiyo imegeuka na sasa amekuwa mmoja wa wachezaji wafumaniaji nyavu maarufu na
sitashangaa endapo ataendelea hivyo akija kuibuka kuwa mchezaji bora wa mwezi
baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne pekee.
Simba wanaonekana
kuwa wazuri zaidi kwa mipira iliyokufa kama vile kona , adhabu ndogo na kubwa
ambapo zaidi ya asilimia 75 ya magoli yao yametokana na mipira iliyokufa. Jambo
jema kwao ni ujio wa kiungo Muzamiru Yassin ambaye licha ya kuuanza vizuri
msimu wake wa kwanza akiwa na Simba sasa amekuwa akiingia mara kwa mara katika
orodha ya wafungaji wa magoli ya Simba na kuongeza idadi ya wafungaji kutoka kila eneo la uwanja nje ya eneo la
ushambuliaji.
Bado Simba
wanakabiliwa na changamoto ya watu wabunifu katika eneo la mwisho la kumalizia
langoni mwa wapinzani wao hasa utoaji wa pasi za mwisho, licha ya kuwa na na
watu wenyenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kuuchezea.
Kwa upande wa Yanga
ushirikiano mkubwa walionao wachezaji unaonekana kuwapa nafasi na uwezo wa
kufanya vizuri zaidi katika ligi hii, jambo la kufurahisha ni kuona jinsi ambavyo Chirwa na Msuva wanaelewana
sana kwani magoli matatu kati ya matano ya Chirwa yamepikwa na Msuva.
Pamoja na ugumu wa ligi hii inaonekana wazi kuwa ina
msisimko wa aina yake hasa kwa wapinzani wa jadi wa soka letu Simba na Yanga, ambao bila shaka mmoja wao
ndiye atakayekuwa bingwa wa ligi hiyo.
Simba wakijvunia uwezo wao wa kuuchezea mpira hasa katika
eneo la kiungo na uwezo wa kucheza pasi fupi fupi na kupanga mashambulizi kwa
kutumia wachezaji wao wa pembeni kama Kichuya na Mnyate ili kuzipa presha safu
za ulinzi kwa timu wanazokutana nazo.
Yanga wakivunia
ubunifu wa viungo kama Niyonzima na Kamusoko lakini pia wamekua wakitegemea
spidi ya washambuliaji wao Chirwa, Msuva na Ngoma ambao ni ngumu sana kuwazuia
pale wanapofanya mashambulizi ya
kushtukiza langoni mwa adui.
Huwezi kumsahau
Tambwe ambaye kwa kawaida anapokuwa ndani ya eneo la sita katika lango la
mpinzani anajua ni nini cha kufanya na hasa anapokuwa na watu waliomzunguka
wanaojua majukumu yao hasa katika eneo la kiungo.
Kwa ujumla vikosi vya
timu zote mbili ni vikosi vinavyowahakikishia ubingwa endapo wataweza kutunza
mwenendo wao katika ligi.
Idadi ya magoli wanayofunga kwenye mechi zao ni
dalili tosha ya kuonyesha kuwa wana kitu
wanachokitafuta katika ligi hii ni jam,bo la kusubiri na kuona
Post a Comment