Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

RAIS DKT. MAGUFULI ALAKIWA SALAMA NA RAIS MH. UHURU KENYATA.

 Rais Dkt John Pombe Magufuli, akipokelewa  na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta alipokaribishwa Ikulu, Nairobi nchini Kenya hii leo. 

Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya.

Na Joseph Peter.
Rais Magufuli amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao wamefanya mazungumzo rasmi.


Wakizungumza na wanahabari baada ya kumaliza mazungumzo yao ya faragha kwenye ikulu ya Nairobi, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo na kufanyia kazi changamoto zilizopo.
Rais Magufuli amesema amemuhakikishia Rais Kenyatta kuendelea kushirikiana nae katika masuala ya maendeleo na kwamba kama ndugu hakuna suala ambalo watashindwa kulipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake Rais Kenyatta, amesema kuwa, pamoja na kuwa kuna masuala ambayo viongozi hao hawakuweza kuyapatia ufumbuzi kwenye mazungumzo yao, jitihada zinaendelea ili kupata muafaka.
Viongozi hawa wawili pia wamewaagiza mawaziri wao wa mambo ya nje, Amina Mohamed wa Kenya na Augustin Mahiga wa Tanzania, wakutane mwishoni mwa mwaka huu kuzungumzia masuala ambayo yamesalia na yanahitaji kupatiwa ufumbuzi.
Miongoni mwa masuala ambayo watu wengi walitarajia kuona viongozi hawa wakiyaweka wazi kwenye mkutano wao na waandishi wa habari, hayakuwekwa wazi kama ilivyotarajiwa jambo ambalo limeendelea kuibusha maswali kuhusu maeneo kadhaa ambayo nchi hizi zinavutana.
Itakumbukwa kuwa suala la watalii kuingia nchini Tanzania lilikuwa ni suala lililoibusha sintofahamu kubwa mwaka jana na hadi sasa, huku pia uhuru wa raia wa Kenya kuingia Tanzania bila kubugudiwa ni suala jingine ambalo halikuzungumzwa na viongozi hawa
Hata hivyo katika kutuliza sintofahamu hii, viongozi hawa wamewahakikishia raia wao kutokuwa na hofu, na kwamba tayari masuala kadhaa yameanza kupatiwa ufumbuzi na makubaliano yake yatatangazwa hivi karibu.
Rais Magufuli pia akasifia namna ambavyo amefanikiwa kupunguza suala la ukiritimba na rushwa Serikali, jambo ambalo amemuomba Rais Kenyatta kulishughulikia ipasavyo kwakuwa linakwamisha maendelo ya nchi.

Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.

 Rais Magufuli yupo nchini Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo kesho anahitimisha ziara yake kisha atarejea jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride la Jeshi la Kenya

Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta.





No comments

Powered by Blogger.