Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

ACT WAZALENDO WATOA TAMKO



Na: Jumanne Juma, Dar es salaam


Chama cha ACT-Wazalendo leo kimetoa tamko kwa umma wa watanzania na likilenga utekelezwaji wake na  rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Drt: John Pombe Mgufuli juu ya mambo matatu likiwemo kukandamizwa kwa uhuru wa kujieleza hapa nchini.
Tamko hilo limekuja baada ya wajumbe wa chama cha ACT-Wazalendo wakiongozwa na Naibu katibu mkuu bara Ndugu Msafiri Mtemelwa, kufanya ziara ya kukagua uhai wa chama kwenye mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mkoa wa kichama Kahama na Tabora kuanzia tarehe 24 hadi 31 octoba 2016.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari katika makao mkuu ya chama hicho jijini dar es salaam leo, katibu wa itikadi, mawasiliano na uenezin Ado Shaibu amesema kuwa chama cha ACT-Wazalendo wameamua kutoa tamko hilo kwa maslai ya taifa.
Akizungumzia  suala la watoto wa masikini kutelekezwa kwenye ugawaji wa mikopo ya elimu ya juu, huku wakipinga utaratibu wa sasa wa utoaji wa mikopo wa elimu ya juu ambao ukiachwa bila kupingwa utawafanya watoto wengi kutoka familia masikini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo.
Amesema ili kuepuka suala hilo na kuwasaidia watoto wa masikini hapa nchini haina budi serikali kuweka mfumo wa scholarship na kozi nyingine zilizobaki ziende kwa mfumo wa mikopo na kuwakumbusha vijana kupigania mikopo ambayo ni haki yao ya msingi.
Amesema hali hii inathibitishwa na takwimu zilizotolewa na bodi ya mikopo ambapo kati ya wanafunzi takribani 65000 wenye sifa ya kujiunga na elimu ya juu, ni takribani wanafunzi 20000 pekee ndio waliopata mikopo, ikiwa ni kinyume na ahadi za Rais Magufuli alizozitoa wakati wa kampeni zake kuwa hakuna mwanafunzi atakaefaulu kwenda chuo kikuu ambae atashindwa kujiunga na elimu hiyo kwa kukosa mkopo.
Shaibu ameongeza kuwa tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano hapa nchini kumekuwepo na ukandamizwaji mkubwa wa uhuru wa kujieleza na serikali ya chama cha mapinduzi, na chama kimekuwa na jitihada za makusudi kupinga muswada wa huduma za habari, kimaudhui muswada huo ni jitihada nyingine za serikali ya awamu ya tano kuzika uhuru wa mawazo baada ya kujaribu kudhibiti shughuli halali za vyama vya siasa.
Amesema kama muswada huo utapitishwa na kuwa sheria basi utampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya habari kupitia kifungu cha 55 kuzuia uchapishwaji wa habari yoyote au kufungia chombo cha habari kwa kigezo cha kutishia usalama wa taifa, akiongeza kuwa uzoefu unaonyesha madaraka haya yanapoachwa mikononi mwa waziri yamekuwa yakitumiwa kuviziba mdomo vyombo huru vinavyoikosoa serikali.
Chama cha ACT-Wazalendo wanaungana na jukwaa la wahariri wa vyombo vya habari(TEF) kupinga uwasilishwaji wa haraka wa muswada huo bila ushirikishwaji mpana wa wadau wa sekta ya habari ili kufanyiwa maboresho.
Suala la mwisho ambalo limezungumziwa na chama hicho hii leo ni pamoja na uungwaji mkono wa chama hicho wa kufufua ajenda ya katiba mpya, kwa kuwa bado wananchi wengi hapa nchini wanahitaji katiba mpya , na chama kina malengo ya kuendelea kupigania ajenda ya katiba mpya kwenye harakati zake mbalimbali za kisiasa.
Kwa ujumla viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo wamesisitiza umuhimu wa chama kuendelea kujikita katika siasa za masuala ya kuwatetea wanyonge na kutoyumbishwa na propaganda za wale wanaotaka kuwatoa kwenye mstari.

1 comment:

  1. Kazi nzuri naamini hiki ni Chama mbadala wa uhakika.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.