WIZARA YA ARDHI YAWEKA WAZI TARATIBU ZA UTHAMINI WA FIDIA NCHINI
Na: Imani Kelvin Mbaga
Evelyne Mugasha Kaimu Mthamini Mkuu wa Serikali |
Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa ufafanuzi juu ya utaratibu unaotakiwa
kutumika kabla, wakati na baada ya kufanya tathmini ya ardhi na mali isiyohamishika
ili kuondoa malalamiko wakati wa kulipa fidia.
Akiongea na waandishi
wa habari katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam leo, kaimu
mtathmini mkuu wa serikali, Evelyne Mugasha, alisema uwazi katika ufanyaji wa
tathmini utasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi hasas wakati wa kufanya
tathmini kabla ya kulipa fidia.
“tumefanya
tathmini nchi nzima ili kujua gharama ya ardhi kwa nchi nzima, hata hivyo
taratibu za kufanya tathmini ziko wazi tena zipo kisheria na siyo suala la
kubahatisha, ingawa malalamiko ya wananchi wengi yanatokana na kutojua taratibu”
Alisema Mugasha.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa mbele ya waandishi wa habari na wawakilishi kutoka
wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kitengo cha uthamini, zipo
taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kulipwa fidia kwa mtu
yeyote ambaye ardhi yake imefanyiwa tathmini hasa pale inapohitajika kwa
matumizi kama vile ya uwekezaji.
Wawakilishi kutoka wizara ya ardhi kitengo cha uthamini wakiongea na waandishi |
Baadhi ya
mambo ya msingi kwa mfidiwa ni kama aina mabalimbali za posho anazostahili
kulipwa kama vile posho ya usumbufu, posho ya upotevu wa makazi, posho ya
upotevu wa faida, posho ya usafiri ikiwa pamoja na gharama za awali za kupata
ardhi.
“ULIPAJI WA
FIDIA: Fidia inaweza kulipwa kwa pesa taslim au kwa mfumo wa hundi. Ulipaji hufanywa
na wahasibu wa mlipaji fidia kwa kushuhudiwa na Mtendaji wa mtaa/kijiji anaye
wathibitisha walipwaji fidia, Mthamini anapaswa kuwepo kushuhudia nyaraka za
uthamini walizoachiwa wananchi wakti wa uthamini (mf.Fomu Na 69)” Ilisema
sehemu ya taarifa hiyo.
Mugasha pia
alisistitiza kuwa uthamini ni taaluma hivyo ni lazima wananchi waiheshimu na
kuwaamini wathamini huku akiainisha sheria na miongozo inayoongoza taaluma na
huduma ya uthamini kama vile Sheria ya ardhi No 4 & 5 za mwaka 1999, Kanuni
za Sheria za ardhi za mwaka 2001, Sheria ya utwaaji Na 47 ya mwaka 1967 na
Waraka Na 1 wa Baraza la mawaziri.
Post a Comment