Aliyekuwa mlinzi wa maslahi ya umma
nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela ametawazwa kuwa mtu mashuhuri zaidi
wa Forbes wa mwaka 2016.
Bi Madonsela aliwashinda marais watatu
wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wan chi ya Rwanda
katika kushinda tuzo hiyo.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec.
Bi Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa
Nairobi Alhamisi jioni, amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya
ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika
Kusini. Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa
miaka sita.
Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani, Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.
Aliwahi
kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom
Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga
mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia
tajiri ya Gupta.
Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.
Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili, Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Huu ni mwaka wa sita kwa tuzo hiyo ya Forbes kwa mtu mashuhuri zaidi Afrika kutoleewa.
Washindi wa awali ni:
2011 - Sanusi Lamido Sanusi, aliyekuwa wakati huo Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria.
2012 - James Mwangi, CEO wa Benki ya Equity, Kenya
2013 - Akinwumi Adesina, aliyekuwa wakati huo Waziri wa Kilimo Nigeria.
2014 - Aliko Dangote, mwenyekiti wa CEO wa kampuni ya Dangote Group, Nigeria.
2015 - Mohammed Dewji, CEO wa kampuni ya MeTL Group, Tanzania
Post a Comment