WIKI YA KIFO KATIKA LIGI MBALIMBALI BARANI ULAYA
Na: Imani Kelvin Mbaga
Baada ya
ligi mbalimbali kwenda mapumziko kupisha michezo ya timu za taifa, ratiba ya
ligi hizo imerudi tena na mwishoni mwa juma hili kutakuwa na michezo mingi
itakayochezwa.
Huko barani
Ulaya hususani katika ligi kubwa tano zinazotazamwa na kufuatiliwa na watu
wengi zaidi duniani, katika ligi nne hii ni wiki ya kifo ambapo michezo mikubwa
inayosubiriwa takribani msimu mzima na mamilioni ya mashabiki inatarajiwa
kuchezwa.
Mamilioni ya
mashabiki wana hamu kubwa ya kuona ufundi, mbinu, rekodi na hata vituko ikiwa
ni pamoja na tambo toka kwa makocha, wachezaji na hata wapenzi wa vilabu vyote.
LIGI YA ENGLAND “EPL”-Manchester
United Vs Arsenal
Hapa
kutakuwa na mchuano mkali kati ya Manchester United wanaowakaribisha washika
bunduki wa jiji la London Arsenal katika uwanja wao wa Old Trafford.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao |
Mechi hii
inachezwa wakati timu hizi zikiwa na nafasi tofauti katika msimamo wa ligi
ambapo Arsenal wako katika nafasi ya nne huku Manchester United wakiwa katika
nafasi ya sita wakiwa na tofauti ya pointi sita.
Takwimu zinaonyesha
kuwa katika michezo mitano iliyopita kwa vilabu hivi kukutana kila timu
imeshinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja. Lakini ikumbukwe kuwa
kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger hajawahi kumfunga kocha wa Manchester
United Jose Morinho katika mchezo wowote wa ligi
Wakati
takwimu hizo zikishindwa kutoa mwelekeo kila klabu kati ya hivi viwili msimu
huu inaonyesha katika michezo mitano ya mwisho katika mashindano yote
Manchester United wamepoteza michezo miwili, wameshinda miwili na kutoka sare
mchezo mmoja.
Paul Pogba na Jesse Lindgaard wachezaji wa Man Utd |
Arsenal kwa
upande wao katika michezo mitano iliyopita wametoka sare mbili na kushinda
michezo mitatu. Lakini pia toka ligi hii ianze kuchezwa jumla ya michezo 11
imechezwa na Arsenal wamepoteza mchezo mmoja pekee siku ya ufunguzi. Wakati
United wameshapoteza mitatu
LIGI YA UJERUMANI
“BUNDES LIGA”- Bayern Munchen Vs Borussia Dortmund
Katika
Bundes liga mabingwa watetezi Bayern Munchen watasafiri kwenda Signal Iduna Park kuwavaa Borussia
Dortmund baada ya michezo kumi ya ligi. Timu hizo zinakutana huku mabingwa hao
watetezi, Bayern Munchen wakiwa wanaongoza ligi hiyo baada ya kushinda michezo
saba na kutioa sare michezo mitatu wakati wenyejio wao wao Dortmund tayari
wameshapoteza michezo miwili na kushinda michezo mitano na sare tatu
Kivutio
kikubwa ni takwimu zao zinazoonyesha kuwa Bayern wameshinda jumla ya mechi 20
kati ya mechi 40 walizokutana wakati ambapo Dortmund wameshinda michezo 13 na 7
kati ya hiyo 40 ikiamuliwa kwa sare.
LIGI YA HISPANIA “LA
LIGA”
Mechi
nyingine yenye mvuto wa kipekee mwishoni mwa juma hili ni mechi kati ya Real
Madrid na jirani zao Atletico Madrid mechi itakayochezwa pale Estadio Vicente Calderon uwanja wa nyumbani
wa Atletico Madrid.
Atletico Madrid wakiwa na furaha baada ya kufunga goli |
Katika miaka
ya hivi karibuni upinzani kati ya watani hawa wa jadi umenogeshwa zaidi na
namna Atletco Madrid wanavyofanya vizuri katika michuano ya ya ndani na ile ya
barani Ulaya kwani katika kipindi cha miaka mitatu watani hawa wa jadi
wamekutana mara mbili katika fainali za klabu bingwa barani humo huku mara zote
real Madrid wakiibuka kidedea.
Takwimu
zinaonyesha kuwa timu hizi zimeshakutana mara 41 wakati ambapo Real Madrid wakionyesha
kuwawanyasa sana watani wao kwa kuibuka na ushindi mara 24 dhidi ya mara 7
pekee walizoibuka Atletico na wameshagawana point mara 10.
Real Madrid katika chereko chereko za ushindi |
Wanaingia
uwanjani baada ya michezo 11 ya ligi ambapo Real wao hawajapoteza mchezo wowote
na wameshinda michezo minane na kutoka sare michezo mitatu, na kuongoza ligi
wakati watani wao wameshapoteza michezo miwili na katika msimamo wanashikilia
nafasi ya 4.
LIGI YA ITALIA “SERIE A”-
AC Milan Vs Inter Milan
Ac Milan
wakiwa katika nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi na tayari msimu huu wameshapoteza
michezo mitatu kati ya michezo 12 waliyocheza watakuwa wakiikaribisha Inter
Milan ambao katika michezo 12 ya ligi msimu huu tayari wamepoteza michezo
mitano na wamejikirta katika nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi hiyo.
Ac Milan wakishangilia moja ya mabao waliyofunga |
Mchezo huu
utachezwa Jumapili katika dimba la uwanja wa San Sirro na tayari timu hizi
zimeshakutana mara 34 wakati Ac Milan wakiibuka wababe mara 16 dhidi ya 14 ya watani
wao na mara 4 wakigawana pointi.
Bila shaka
hii itakuwa ni michezo yenye mvuto licha ya kuathiriwa na uwepo wa majeruhi
wengi katika vikosi mbalimbali vya timu zitakazocheza hiyo kesho na kesho
kutwa.
Kama kawaida
michezo hii inakzikutanisha timu zinazoongozwa na makocha wanaotumia zaidi
ufundi dhidi ya timu zinazoongozwa na makocha wanaotumia zaidi mbinu
KOCHA
|
TIMU(MBINU)
|
Vs
|
KOCHA
|
TIMU(UFUNDI)
|
UWANJA
|
JOSE
MORINHO
|
MAN UTD
|
Vs
|
ARSENE
WENGER
|
ARSENAL
|
OLD
TRAFFORD
|
DIEGO SIMEON
|
ATLETICO
MADRID
|
Vs
|
ZINEDIN ZIDANE
|
REAL MADRID
|
VICENTE CALDERON
|
THOMAS TUCHEL
|
BORUSSIA DORTMUND
|
Vs
|
CARLO ANCELOTI
|
BAYERN MUNCHEN
|
SIGNAL IDUNA PARK
|
VICENZO MONTELA
|
AC MILLAN
|
Vs
|
STEPHANO PIOLI
|
INTER MILAN
|
SAN SIRRO
|
Hata hivyo
timu kama Ac Millan na Inter Millan ziko wakati wa mpito kujaribu kurejesha
makali yao ya miaka iliyopita na hivyo inawezekana kabisa mechi yao itakuwa ni
mechi itakayotaliwa zaidi na mbinu kwa mabenchi yote mawili ya ufundi kwani
lengo namba moja ni kutafuta ushindi kabla ya kuangalia umechezaje.
Post a Comment