SAMATTA KUTUA KUWAKABILI ZIMBABWE
Na: Imani Kelvin Mbaga
Mbwana Samatta nahodha wa Taifa Stars |
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania anaechezea klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana
Ally Samatta, anatarajiwa kuwasili leo saa sita usiku kujiunga na kikosi cha
timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kilichoweka kambi katika hoteli ya
Urban Rose jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi
ya timu ya taifa ya Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa shirikisho la soka nchini Alfred Lucas,
ilisema kuwa, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania atakuja kuungana na
wenzake ili kujiandaa na mechi hiyo muhimu kwa lengo la kupata ushindi ili
kuinua viwango vya timu ya taifa katika msimamo wa ubora unaotolewa kila mwezi
na shirikisho la soka la kimataifa, FIFA.
Wachezaji
wengine walioitwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Boniface Mkwasa ni
Deogratius Munishi –Young Africans
Said Kipao –JKT Ruvu
Aishi Manula –Azam FC
Mabeki
Erasto Nyoni -Azam FC
Michael Aidan -JKT Ruvu
Mwinyi Haji -Young Africans
Mohamed Hussein –Simba SC
David Mwantika -Azam FC
James Josephat –Tanzania Prisons
Vicent Andrew -Young Africans
Viungo wa Kati
Himid Mao -Azam FC
Mohammed Ibrahim –Simba SC
Jonas Mkude –Simba SC
Muzamiru Yassin –Simba SC
Viungo wa Pembeni
Abdulrahman Mussa -Ruvu Shooting
Shiza Kichuy –Simba SC
Simon Msuva -Young Africans
Jamal Mnyate –Simba
Washambuliaji
Ibrahim Ajib –Simba SC
John Bocco -Azam FC
Mbwana Samatta -K.R.C Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli –Oman
Thomas Ulimwengu –Mchezaji huru
Omar Mponda -Ndanda
Hii itakuwa
ni mechi muhimu sana kwa timu ya taifa kutokana na nafasi iliyopo katika
msimamo wa ubora duniani kwa mujibu wa FIFA
Post a Comment