TWIGA KAMILI YAIFUATA CAMEROON
Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars |
Na: Imani Kelvin Mbaga
Kikosi cha
wachezaji 17 na viongozi wanne cha timu ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga
Stars, kimeondoka leo kwenda nchini Cameroon kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya
kimataifa na timu ya taifa ya wanawake ya nchi hiyo kufuatia mwaliko waliopata kutoka
shikirisho la soka la Cameroon, FECAFOOT.
Akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo msemaji wa shirikisho la soka la
Tanzania, Alfred Lucas, alisema timu hiyo inatarajiwa kutua jijini Younde
baadae leo na kwamba kikosi cha wachezaji hao 17 kitakuwa huko kuliwakilisha
taifa pamoja na kupata kipimo halisi kujiandaa na michuano mbalimbali.
Hata hivyo
Lucas alisema wachezaji 20 waliitwa tayari kwa ajili ya mechi hiyo lakini
wachezaji watatu kati yao wameshindwa kusafiri na timu kwa sababu mbalimbali
ikiwemo majeruhi na kuchelewa kwa visa.
“Mwalimu
aliita wachezaji 20 wa timu yetu ya Twiga Stars, lakini kwa bahati mbaya
wachezaji 17 pekee ndiyo wameondoka na timu hiyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo
kuchelewa kwa viza, hata hivyo kwa kuwa ni mchezo mmoja tu wa kirafiki,
kukosekana kwao hakutaathiri kikosi kwa jumla” Alisema Lucas.
Msemaji huyo
aliwataja wachezaji hao kuwa ni
Walinda mlango:
Fatma Omary
Najiat Abas
Walinzi
Wema Richard
Sophia
Mwasikili (nahodha)
Anastazia Katunzi
Fatma Issa
Maimuna
Hamiss
Happiness
Mwaipaja
Marry
Massatu
Viungo
Donisia
Minja
Amina Ally
Situmai
Abdallah
Anna
Mwaisula
Fadhila
Kigalawa
Washambuliaji
Fatma Swaleh
Asha Rashid “Mwalala”
Mwanahamisi
Omary
Viongozi
waliosafiri na timu hiyo ni pamoja na
Sebastian
Nkoma (kocha mkuu)
Edna
Lema(kocha msaidizi)
Eliutel
Mollel
Wakati ambapo
mwenyekiti wa soka la wanawake Amina Kaluma anatarajia kuondoka kesho kujiunga
na timu hiyo.
Post a Comment