Your Business Looks Here

Your Business Looks Here
tupo kwenye tathimini ya mwaka radio itarudi hewani kuanzia tarehe 25

WAZIRI POSSI ASISITIZA HALMASHAURI ZOTE KUTEKELEZA AGIZO LA KUUNDA KAMATI ZA WATU WENYE ULEMAVU

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu alipofanya ziara ya kikazi.



Na. Mwandishi Wetu


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amezitaka Halmashauri zote nchini kutekeleza agizo la kuunda Kamati za Watu Wenye Ulemavu kuanzi ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.

Mhe. Possi ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika mikoa ya Mwanza na Simiyu hivi karibuni ambapo alitembelea makazi ya watu wenye mahitaji maalum ya Bukumbi, Shule ya watu wenye mahitaji maalum ya Mitindo na kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi.

Kauli ya Dkt. Possi imekuja kufuatia maagizo yaliyolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka huu kwa kuziandikia Halmashauri zote kutekeleza uundwaji wa kamati za Watu wenye Ulemavu ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.

“Ni muhimu sana kutekeleza agizo lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwanzoni mwa mwaka huu ambalo limeeleza wazi kuundwa kwa Kamati za Watu wenye Ulemavu na ikumbukwe kuwa, suala hii lipo kisheria na lina miongozo yake katika utekelezaji wake”. Alisema Waziri Possi.

Waziri Possi alisisitiza kuwa maagizo ya kuundwa kwa kamati za watu wenye ulemavu yalitolewa na Ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji sahihi wa taarifa za watu wenye ulemavu ili kupata namna bora ya kutatua changamoto zinazowakabili.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa agizo hilo ili kusaidia kujua mahitaji ya watu wenye ulemavu na kuwa na njia nzuri za utatuzi wa changamoto zao kwa kuzingatia takwimu sahihi zitakazo toa picha halisi ya hali zao katika nyanja zote.”Alisema Dkt.Possi

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa vipaumbele kwa watu wenye ulemavu na mahitaji maalum kwa kuwapa nafasi za ushiriki katika mipango yote ya maendeleo ikiwemo; elimu, huduma za afya na uchumi ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha katika jamii.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda alimpongeza Mhe. Possi kwa juhudi za kuhakikisha sauti za watu wenye ulemavu zinasikika katika ngazi zote kwa kuudwa kwa kamati hizo zitazotatua na kutibu changamoto za watu wenye ulemavu.

”Nikupongeze Mhe. Waziri kwa kutembelea Wilaya yetu na kuona umuhimu wa kuweka msisitizo wa uundwaji wa Kamati hizi, nasi tunakuhaidi kulitekeleza hilo kama Ofisi yako ilivyoekeza ili kufikia malengo ya Serikali katika kuhakikisha Haki na Usawa unakuwepo kwa watu wote bila kujali hali zao”.Alisema Mhe.Sweda.



No comments

Powered by Blogger.