MKWASA KATIBU MKUU MPYA YANGA
makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga (kulia) akimtambulisha katibu mkuu mpya wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa (kushoto) |
Na Imani Kelvin Mbaga
Mabingwa
watetezi wa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara, klabu ya Yanga ya jijini Dar es
salaam, imemteua nahondha na kocha wake wa zamani, Charles Boniface Mkwasa
maarufu kama “Master” kuwa katibu mkuu mpya wa klabu hiyo kwa muda wa miaka
miwili.
Akitangaza
uteuzi huo mbele ya waandishi wa habari, katika makao makuu ya klabu jijini Dar
es salaam, makamu mwenyekiti wake, Clement Sanga alisema baada ya uongozi
kutafakari kwa kina wameona kuwa Mkwasa ni mtu sahihi wa kuifanya kazi hiyo.
Charles Boniface Mkwasa, katibu mkuu mpya wa Yanga |
“Mkwasa ni
mchezaji wetu wa zamani na uzoefu wa soka la Tanzania kwa kuwa amelitumikia
katika ngazi za juu, naamini uzoefu wake utatusaidia kuipeleka klabu mbele”
Alisema Sanga
Sanga pia
alisema hii inaweza ikawa njia mojawapo ya kuwafanya wachezaji wa zamani,
walioutumikia mpira wa nchi hii kujiona kuwa ni sehemu ya familia ya soka la
Tanzania, na kwamba huo unaweza kuwa mwanzo wa Mkwasa na wengine kuingia katika
kada ya uongozi.
Naye kocha
huyo wa zamani alisema anaushukuru uongozi kwa kumpa nafasi nyingine ya
kuitumikia klabu hiyo, na akaahidi kuifanya kazi yake mpya kwa uaminifu, huku
akiwaomba mashabiki na wanachama kuwa watulivu na kushikamana ili waweze
kufanya vizuri.
Mkwasa
ameitumikia klabu hiyo kwa nafasi tofauti, akiwa kama mchezaji, nahodha na kwa
nyakati tofauti amekuwa kocha msaidizi na kocha mkuu, hivyo ni miongoni mwa
wanachama wanaoufahamu vema utamaduni wa klabu hiyo.
Wakati huo
huo makamu mwenyekiti huyo amtolea ufafanuzi juu ya klabu yake kukataa kucheza
mechi ya kirafiki na mabingwa wa Afrika kwa upande wa vilabu, timu ya Mamelodi
Sundown kutoka nchini Afrika ya kusini, ambao wapo nchini kupiga kambi ya siku
nne.
Sanga
alisema kuwa benchi lao la ufundi ndilo lililokataa kucheza mechi hiyo, kwa
sababu ya mazingira na ratiba ya ligi inayoendelea, kwakuwa wanakabiliwa na
kibarua cha kuutetea ubingwa wao,kwa mechi zilizopo mbele, ambapo watacheza na
Stand united katika mchezo unaofuata.
Post a Comment